Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto mmoja kati ya watano CAR ni mkimbizi: UNICEF

Mtoto mmoja kati ya watano CAR ni mkimbizi: UNICEF

Wakati hali ikiendelea kutengamaa zaidi ya watu 850,000 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, nusu yao wakiwa ni watoto wanaendelea kukimbia, ama kama wakimbizi wa ndani au wanaokimbilia nchi jirani limesema leo shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Kwa mujibu wa Christophe Boulierac, msemaji wa shirika hilo tarehe 17 mwezi huu maafisa wa misaada watakutana nchini CAR na Brussel Ubelgiji .

Leo ni kutoa taarifa kuhusu hatua zilizopigwa kurejea katika hali ya kawaida, lakini pia kusaka fedha zaidi kufanikisha mchakato huo. Ameongeza kuwa hali ya watoto CAR bado ni tete na hususani kwa mustakhbali wao

(SAUTI CHRISTOPHE BOULIERAC)

“Zaidi ya theluthi moja ya watoto CAR hawaendi shule, asilimia 41 walio chini ya miaka mitano wanautapia mlo uliokithiri, na watoto kati ya elfu sita na elfu kumi wanakadiriwa kuingizwa jeshini na makundi ya wapiganaji tangu mwaka 2013.”