Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mila ni kikwazo kwa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana na wavulana Afrika

Mila ni kikwazo kwa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana na wavulana Afrika

Wazazi barani Afrika hawawezi kuzungumza wazi na watoto wao kuhusu mahusiano ya ngono kwa sababu ya vikwazo vya mila na desturi, amesema mke wa Rais wa ufalme wa Lesotho.

Bi Mathato Mosisili amehudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa wake wa Marais kutoka Afrika uliofanyika kandoni mwa kikao cha baraza kuu cha 71 na kujikita katika afya ya uzazi kwa wasichana vigori katika bara hilo, yeye ni mjumbe wa shirika la wake wa marais dhidi ya HIV na ukimwi, OAFLA.

Miongoni mwa mada walizojadili ni pamoja na mimba zisizotarajiwa, mahusiano ya kimapenzi, ndoa za utotoni na shinikizo rika, kama baadhi ya mambo yanayoathiri wasichana vigori. Na Bi Mosisili anasema ukosefu wa mawasiliano unafanya hali kuwa mbaya zaidi

(SAUTI BI MOSISILI)

“Hakuna mawasiliano ya kutosha baina yetu sisi kama wazazi na wao kwa sababu ni kundi lingine kabisaa, na matokeo yake sisi kama wazazi hatuelewi kinachowasibu”