Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda ya nishati imegusa maeneo ya jamii za chini- Museveni

Ajenda ya nishati imegusa maeneo ya jamii za chini- Museveni

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amehutubia mjadala wa wazi wa mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa yeye anafurahia sana mada kuhusu maendeleo endelevu na kubadili maisha, ambayo ndiyo maudhui ya kikao hicho.

Amesema mada hiyo imekuja wakati sehemu ndogo ya dunia inafurahia utajiri ilhali maeneo mengi duniani yanaathirika na umaskini.

Hata hivyo amesema kuna nuru kwani bara Afrika lina watu takribani milioni 414 walioondokana na umaskini akisema..

(Sauti yaYoweri)

“Uganda mwaka 2004 asilimia 56 walikuwa wanaishi katika umaskini, lakini hivi sasa idadi hiyo ni asilimia 19 na nina matumaini kuwa ifikapo mwaka 2017 itafikia asilimia 10. Na je  dunia sasa ni bora zaidi kwa huu utajiri huu mpya unaonufaisha karibu ulimwengu mzima.”

Kuhusu malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs amesema ..

(Sauti ya Yoweri)

“Tuna furaha kuwa hatimaye, ajenda ya dunia hivi sasa inagusa viambato ambavyo ni muhimu katika kuleta mabadiliko kwa jamii zilizochochea mapinduzi ya viwanda, hususan kujumuishwa kwa nishati katika orodha ya SDG, kumeondokana na ajenda ya zamani.”