Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utalii umekuwa ni pasi ya safari ya mafanikio na amani: Ban

Utalii umekuwa ni pasi ya safari ya mafanikio na amani: Ban

Kukiwa na takribani watu bilioni 1.2 wanaosafiri kila mwaka, utalii umekuwa ni sekta muhimu katika uchumi, pasi ya kuelekea mafanikio na amani, na ni msukumo wa kuleta mabadiliko katika kuboresha maisha ya mamilioni ya watu.

Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya utalii, ambapo amesema kila mtu ana haki ya kupata burudani na huduma ya utalii kwa misingi sawa.

Ameongeza kuwa hata hivyo watu bilioni 1 duniani kote wanaoishi na ulemavu, pamoja na watoto wadogo, wazee na watu wenye mahitaji mengine bado wanakabiliwa na vikwazo katika kupata mambo muhimu ya kusafiri kama vile habari za wazi na kuaminika, usafiri wenye ufanisi na huduma za umma, na mazingira ambayo yatawarahisishia kusafiri.

Hata pamoja na teknolojia ya kisasa, wale walio na ulemavu wa macho, kusikia, uhamaji au upungufu wa utambuzi ni kuwa kushoto nyuma katika nchi nyingi za utalii. Licha ya teknolojia amesema wengi wenye matatizo kama ya kuona, wasiosikia  na viwete bado wanaachwa nyuma katika maeneo mengi ya utalii.

Ban ameongeza kuwa fursa ni muhimu sana kwa soko na sera za utalii endelevu. Siku ya kimataifa ya utalii, huadhimishwa kila mwaka Septemba 27.