Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Boko Haram yasambaratisha watoto ziwa Chad:UNICEF

Boko Haram yasambaratisha watoto ziwa Chad:UNICEF

Miaka ya machafuko ya kundi la Boko Haram kwenye bonde la ziwa Chad yamesababisha hali ya kibinadamu kubwa mbaya zaidi hasa kwa watoto katika ukanda huo wa Afrika.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, machafuko hayo yamewatawanya watoto milioni 1.4 na kuwaacha wengine takribani milioni wakiwa wamekwama katika maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia.

Christopher Boulierac ni msemaji wa UNICEF..

(SAUTI BOULERAC)

Mgogoro wa ziwa Chad ni mgogoro wa watoto ambao unapaswa kuwekwa katika ajenda ya juu ya kimataifa kuhusu kutawanywa na uhamiaji,Mahitaji ya kibinadamu yanazidi uwezo wa kuyakabili hususani hivi sasa ambapo maeneo yaliyokuwa hayafikiki awali kuna fursa ya kufika”

Ripoti hiyo ambayo imetolewa kabla ya mkutano wa kimataifa wa umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi na wahamiaji utakaofanyika Septemba 1.