Bei ya mafuta yasiyosafishwa kupanda :Benki ya Dunia

Bei ya mafuta yasiyosafishwa kupanda :Benki ya Dunia

Benki ya Dunia imeongeza utabiri wake 2016 kwa bei ya mafuta yasiyosafishwa kufikia dola 43 kwa pipa kutoka dola 41 kwa kila pipa kutokana na kukatika kwa ugavi na ongezeko la mahitaji katika robo ya pili.

Bei ya mafuta ilipanda kwa asilimia 37 katika robo ya pili yam waka 2016 kutokana na kukatika vikwazo katika usambazaji hususani moto wa porini nchini Canada na hujuma katika miundombinu ya mafuta nchini Nigeria.

Utabiri huo upo katika ripoti mpya ya Benki ya Dunia kuhusu mtazamo wa bidhaa na masoko.