Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiwawezesha wasichana vigori umewezesha jamii:UNFPA

Ukiwawezesha wasichana vigori umewezesha jamii:UNFPA

Katika kuelekea siku ya idadi ya watu ulimwenguni, ambayo kila mwaka huadhimishwa Julai 11, mwaka huu wasicha vigori wamepewa kipaumbele. Kwa mujibu wa shirika la idadi ya watu duniani UNFPA wasichana vigori ambao hukumbwa na changamoto nyingi, hawapewi nafasi wanayostahili kutimiza ndoto zao.

Shirika hilo linasema wengi hukatiza masomo ama kwa kupata mimba, ndoa za utotoni, ukeketaji na sababu nyingine nyingi. Kwa kulitambua hilo UNFPA imetoa kauli mbiu “ukiwezesha wasichana vigori umewezesha jamii” na kutoa wito wa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi zao.

Katika kuhakikisha hilo linatimia shirika hilo litafanya nini? John Mosoti ni mkuu wa kitengo cha masuala ya kimataifa cha shirika hilo

(SAUTI JOHN MOSOTI)