Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi ziongeze ushuru wa tumbaku ili kupunguza matumizi ya watumiaji:WHO

Ongeza Ushuru, punguza vifo .(Picha@WHO)

Nchi ziongeze ushuru wa tumbaku ili kupunguza matumizi ya watumiaji:WHO

Wakati leo ni siku ya kutokuvuta tumbaku duniani, shirika la afya ulimwenguni WHO linasisitiza hatua za kisera zaidi zinazoweza kupunguza matumizi ya tumbaku na hivyo kuokoa uhai wa waathirika wa bidhaa hiyo.

WHO inasema kuwa uvutaji tumbaku unaweza kuua zaidi ya watu Milioni Nane kila mwaka ifikapo mwaka 2030 na hivyo sasa linapendekeza uongeza wa ushuru wa bidhaa hiyo inayosababisha vikfo vya watu Milioni Sita kila mwaka.

Tayari barani Afrika hatua za kisera zimechukuliwa ili kupunguza ushawishi wa matumizi ya tumbaku kwa binadamu.

Takwimu zinaonyesha kuwa ongezeko la kodi kwa asilimia 50 litapunguza wavuta sigara na tumbaku Milioni 49 duniani ndani ya miaka mitatu na hivyo kuokoa uhai wa watu Milioni 11