Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajane wanastahili maisha yenye hadhi na wasibaguliwe: UM

Wajane wanastahili maisha yenye hadhi na wasibaguliwe: UM

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kuchagiza harakati za kutokomeza vitendo vyote vya ubaguzi na unyanyapaa vinavyokabili wajane duniani wakati huu ambapo inakadiriwa kuna wajane Milioni 115 ulimwenguni wakiishi katika maisha ya dhiki. Kaimu Mkuu wa shirika la masuala ya wananake la Umoja wa Mataifa, UN-Women, Lakshmi Puri ametoa kauli hiyo katika ujumbe wake wa siku ya wajane duniani tarehe 23 mwezi Juni akifafanua kuwa maisha ya wajane siyo tu ni ya dhiki bali zaidi ya asilimia Hamsini hukabiliwa na maisha ya vipigo na wakati mwingine kutoka kwa familia zao na wakiwa na umri mdogo wanakabiliwa na unyanyasaji wa kingono. Bi. Puri amesema wajane ni wachangiaji wakubwa katika jamii wakiwa ni mama, walezi na wakuu wa kaya na hivyo haki zao zinapaswa kulindwa ndani ya sheria na sera za kitaifa kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa kutokomeza ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanawake, CEDAW na ule wa haki za mtoto CRC ambao nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeridhia. Alice Wamboi kutokaNairobi,Kenyani mjane  ambaye mume wake alifariki dunia mwaka 2009 na kumuachia watoto watatu na sasa akiwa na miaka 35 anaelezea madhila anayokumbana nayo.  

(SAUTI YA ALICE WAMBOI)