Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukabili mabadiliko ya tabia nchi kunahitaji fedha na ushirikiano:UNEP

Kukabili mabadiliko ya tabia nchi kunahitaji fedha na ushirikiano:UNEP

Mafanikio ya kukabili mabadiliko ya tabia nchi na kufikia maendeleo endelevu Afrika kunahitaji fedha, ushirikiano na ushirikishwaji wa wadau wa asasi zisizo za kiserikali, wameelezwa washiriki wa wakongamano la ngazi ya juu kwa ajili ya kupunguza gesi ya cabon Afrika lililomalizika leo mjini Kigali Rwanda.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa mazingira UNEP, kila nchi inajukumu la kuchagia katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi Afrika. Waziri wa maliasili wa Rwandwa Vicent Biruta mesema maendeleo lazima yawe endelevu, la sivyo sio maendeleo, na yatafikiwa tuu kama mabadiliko ya tabia nchi yatadhibitiwa.

Ameongeza kuwa ushirikiano baiana ya nchi, umma, asasi za kiraia na sekta binafsi ni muhimu sana. Rhoda Peace Tumusiime, Kamishina na Muungano wa Afrika kwa ajili ya uchumi na kilimo vijijini, amepongeza ukweli kwamba nchi zimekuwa na mkakati wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi hata kabla ya mkataba wa Paris wa 2015, lakini amezichagiza kuongeza juhudi.

Wazungumzaji wote katika kongamano hilo wameainisha fursa na haja ya Afrika kuunganisha hatua za kijasiri za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji unaojali mazingira kwa shabaha kubwa ya kufikia agenda ya Umoja wa Afrika ya 2063.