Bila suluhisho majangwa yataongeza uhamiaji

17 Juni 2016

Bila suluhisho la muda mrefu, jangwa na uharibifu wa mazingira hautaathiri upatikanaji wa chakula pekee lakini utaongeza uhamiaji na kutishia uendelevu wa mataifa na kanda mbalimbali amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Katika ujumbe wake katika siku ya kimataifa ya kukabiliana na majangwa yenye kauli mbiu linda dunia, hifadhi ardhi, jumuisha watu, Ban amesema kuwa ili kuepusha madhara ya jangwa ndiyo maana viongozi wa dunia walipitisha kukabiliana na uharibifu wa mazingira kama moja ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Katika hatua nyingine China ikishirikiana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mkataba wa kukabliana na majangwa, wamezindua mkakati wa pamoja wa kukabiliana na majangwa pamoja na kukabiliana na madhara ya ukame ( JAI).

Juhudi hizo zinalenga kuifanya dunia kuwa endelevu ambapo mkakati huo  unatoa muongozo wa kufanya utafiti na kubadilishana ujuzi, taarifa na miradi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter