Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa iko chini ya mashambulizi yanayojumuisha chuki:Zeid

Jumuiya ya kimataifa iko chini ya mashambulizi yanayojumuisha chuki:Zeid

Uwezo wa jumuiya ya kimataifa kutatua mizozo uko chini ya mashambulizi, ameonya kamishina mkuu wa haki za binadamu. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Zeid Ra’ad Al Hussein ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha 32 cha baraza la haki za binadamu kilichoanza mjini Geneva.

Katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 10 ya baraza la haki za binadamu,  Kamishina Zeid amewaambia nchi wanachama  kwamba maadili ya pamoja duniani yanasambaratika, hasa akizungumzia Syria ambako utesaji, watu kuswekwa rumande na uharibifu mkubwa  wa mali na mioundombinu unaendelea. Amesema hali ni ya kusikitisha na kwamba..

(SAUTI YA ZEID)

“Kukusanya na kuchambua taarifa za kutisha, na kuzitolea taarifa , nia ni kuchukua hatua. Lakini zikirundikana na kuishia kwa wenye nguvu , tunaguswa na kutikiswa, tukijihisi wanyonge tusio na msaada kama ambavyo nafikiri wengi duniani wanavyojihisi katika zahma hii.”

Awali waziri wa mambo ya nje wa Uswis Didier Burkhalter ametoa wito wa haki za binadamu kuwa na kujumu kubwa katika miakati ya Umoja wa Mataifa kuzuia mizozo