Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kuzindua filamu ya ustawi wa watoto

UNICEF kuzindua filamu ya ustawi wa watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) kwa kushirikiana na wadau wa filamu  linatarajia kuzindua hii leo  filamu fupi kuhusu ustawi wa watoto iitwayo Mwanzo wa Maisha  inayotarajiwa kusambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii. Grace Kaneiya anatujuza zaidi.

(TAARIFA YA GRACE)

NATS!

Hii ni sehemu ya utangulizi wa filamu hiyo yaani trela kama inayoonyesha watalaamu mbalimbali wakieleza kuhusu watoto na tabia zao, huku pia watoto nao wakionekana katika mambo kadhaa ikiwamo kucheza na mengineyo.

UNICEF imeeleza kuwa muktadha wa filamu hii fupi ya dakika 30 ni kuhusu sayansi ya jukumu la maisha ya mwanzo wa mtoto yanavyoathiri mustakabali  wake kuwa chanya au hasi .

Estela Renner ni mtayarishaji wa filamu hiyo.

(SAUTI ESTEL)

‘‘Tumechukua picha kutoka nchi na  utamaduni tofauti na nilichokibaini ni hisia kila mahali kwamba kila mtu anataka mtoto wake apate kilicho bora kwa kutambua ndoto zake. Lakini pia nimegundua kuwa familia nyingi hazina namna ya kutoa hakikisho hilo.’’

Kenya ni miongoni mwa mataifa yaliyoshirikishwa katika filamu hii.