Maelfu ya watoto bado wanahitaji huduma na msaada baada ya Ebola:UNICEF

Maelfu ya watoto bado wanahitaji huduma na msaada baada ya Ebola:UNICEF

Takribani watoto 23,000 children ambao walipoteza mzazi mmoja au wote, au walezi kutokana na Ebola nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone wataendelea kuhitaji huduma na msaada limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF , wakati likikaribisha tangazo la kutokuwepo visa vipya vya ugonjwa huo Afrika ya Magharibi.

Kudhibiti Ebola ni mafanikio makubwa lakini haitosahaulika athari zilizosababishwa na mlipuko huo kwa nchi hizo tatu amesema Manuel Fontaine, mkurugenzi wa UNICEF wa kanda ya Afrika Magharibi na Kati.

Ameongeza kuwa watu wengi wanaaendelea kutaabika hususani watoto ambao wazazi au walezi wao walikufa na Ebola maisha yao yameachwa ama na ndugu wa familia au walezi na hivyo ni muhimu kuendelea kuwapa msaada zaidi ya huduma za dharura kupitia fedha taslim, shule, mavazi na chakula. UNICEF itaendelea kuunga mkono kampeni za uelimishaji na imetoa ombi la dola milioni 15 ili kufadhili mfuko wa dharura wa Ebola kwa Guinea, Liberia na Sierra Leon kuanzia mwezi huu hadi Machi.