Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumesikitishwa na matamshi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Malawi: OHCRC

Tumesikitishwa na matamshi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Malawi: OHCRC

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imelaani matamashi ya msemaji wa moja ya vyama vikuu vya siasa nchini Malawi ya kwamba wapenziwa jinsia moja kuwa ni wabaya zaidi kuliko mbwa na hivyo wauawe.

Tamko hilo limetolewa mapema mwezi huu na msemaji wa chama hicho Kenneth Msonda, katika ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii na kurudiwa katika mahojiano na vyombo vya habari.

Ofisi ya haki za biandmau imeeleza kuwa Bwana Msonda alishtakiwa kwa kutenda kosa la jinai kwa kuchochea wengine kuvunja sheria na alipaswa kufikishwa mahakamni leo mjini Blantyre baada ya asasi ,mbili za kiraia kumfungulia mashtaka.

Lakini katika hali ya kushangaza mwendesha mashtaka wa serikali aliitaka mahakama kutupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa serikali haimshtaki kiongozi huyo. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa..

(SAUTI RUPERT)

"Tuna wasiwasi kwamba kushindwa kuendesha mashtaka dhidi ya kesi hii kunatuma ujumbe hatari kwamba kushawishi wengine kuua wapenzi wa jinsia moja ni halali na kutakubaliwa na mamlaka za serikali."