Mwendesha mashataka wa ICC ataka Jean-Pierre Bemba afungwe miaka 25

Mwendesha mashataka wa ICC ataka Jean-Pierre Bemba afungwe miaka 25

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imeomba hukumu ya kifungo cha miaka 25 dhidi ya Jean-Pierre Bemba, aliyekuwa mkuu wa kundi la waasi wa Mouvement de Libération du Congo (MLC) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Hatua hiyo inafuatia hukumu iliyotolewa hivi karibuni na mahakama hiyo dhidi ya Bwana Bemba, ambaye alikutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa vita kwa vitendo waasi wake walivyotenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.

Kwenye hotuba yake Bi Bensouda amesema hukumu itakayotolewa itasaidia kutambua mateso yaliyopitiwa na raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati ule, yakiwemo uporaji, mauaji na ubakaji. Amesema pia itatoa mfano ambao utawazuia makamanda wengine kutendea uhalifu kama huo, akiongeza:

(Sauti ya Bi Bensouda)

"Hukumu mnayotarajia kuchukua dhidi ya Bwana Bemba inapaswa pia kusaidia kukemea wazi vitendo vyake vya uhalifu na kuionyesha jamii ya kimataifa msimamo wa mahakama hii wa kukomesha ukwepaji sheria kwa uhalifu huo mbaya ambao husababisha kiasi kikubwa cha mateso na kuharibu ustawi wa jamii."