Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2016 (YPP)

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2016 (YPP)

Kila mwaka, Umoja wa Mataifa hutafuta vijana waliobobea katika fani mbali mbali, ambao wapo tayari kuanza huduma ya kitaaluma kama wahudumu wa kimataifa wa umma. Mpango wa Vijana Waliobobea Kitaaluma, yaani YPP, huleta vipaji vipya kwa Umoja wa Mataifa kupitia kwa mtihani wa kila mwaka.

Mwaka huu wa 2016, mtihani wa kuandika utafanyika mnamo tarehe 14 Disemba, katika fani za Masuala ya Uchumi na, Mifumo ya teknolojia na Habari.

Ili kushiriki mtihani huu, ni lazima uwe unatoka nchi zilizoorodheshwa kushiriki mwaka 2016, uwe na shahada ya kwanza, uwe unaongea Kiingereza au Kifaransa sanifu, na uwe na umri wa miaka 32 kabla ya mwisho wa mwaka huu. Utatakiwa kufanya ombi la kushiriki mtihani huu kati ya tarehe zifuatazo: Mei 19 hadi Julai 19

Kumbuka, itakuwa vyema ikiwa utakamilisha na kuwasilisha maelezo yote kwa njia sahihi na nadhifu kwani hicho kitakuwa kigezo cha kupima uwezo wa wako kukubaliwa kuufanya mtihani.

Kumbuka pia kuwa, maombi ambayo hayatakamilishwa vyema au yatakayochelewa kuwasilishwa hayatakubaliwa, kwa hiyo ni lazima uwasilishe ombi lako kabla ya tarehe ya ukomo.

Kuona kama nchi yako inashiriki, na maelezo zaidi, tembelea tovuti:

http://bit.ly/1aAemgZ

Mtihani

Mtihani umegawika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ambayo ni kwa kuandika, itatahini upana wa ujuzi wako, uwezo wa kutathmini mambo, na uwezo wa kuandika nakala muhimu.

Sehemu ya pili ni kwa wale wanaopita ule wa kwanza pakee, na ni aina ya mahojiano