Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sweden yatoa dola milioni nane kusaidia wakimbizi wa Kipalestina

Sweden yatoa dola milioni nane kusaidia wakimbizi wa Kipalestina

Wakati Shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), linakabiliwa na changamoto za kuhudumia idadi ya wakimbizi inayoongezeka kila siku, serikali ya Sweden imelipiga jeki ya dola million nane kwa ajili ya kuendeleza msaada wake.

Msaada huo uliopokewa kwa mikono miwili na UNRWA, utashughulikia mahitaji ya wakimbizi walioathiriwa na mzozo nchini Syria, kwenye Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Gaza pamoja na maeneo ya Yamouk na Aleppo.

Michael Kingsley-Nyinah Mkurugenzi wa masuala ya UNRWA nchini Syria, amesema, mchango huo unadhihirisha kwamba serikali ya Sweden ijali hatari kubwa inayowakumba wakimbizi nchini Syria na mshirika wa kuweli na UNRWA katika kuhsughulikia wakimbizi.

Kuna zaidi ya asilimia 60 ya wakimbizi 450,000 wa Kipalestina waliosalia nchini Syria ni wakimbizi wa ndani na karibu wote wanategemea UNRWA kwa msaada, wakiwemo wale waliozingirwa katika maeneo yenye mapigano ambako huduma muhimu ni ngumu kufikishwa.