Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kujumuisha makundi yote katika ujenzi wa amani: Kamau

Lazima kujumuisha makundi yote katika ujenzi wa amani: Kamau

Harakati za ujenzi wa amani ni vyema zijumuishe makundi yote ikiwemo makabila madogo,  amesema mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya ujenzi wa amani PCB ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York, Balozi Macharia Kamau. Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami kuhusu maazimio ya aina yake ya ujenzi wa amani baada ya mizozo, yaliyopitishwa leo na baraza la usalama na baraza kuu, Balozi Kamau anaanza kueleza umuhimu wake.