Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali leo zimeweka agano na mustakhbali wa dunia:Ban

Serikali leo zimeweka agano na mustakhbali wa dunia:Ban

Leo hii serikali duniani zimeandika historia kwa kutia saini mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kwa kufanya hivyo zimeweka agano na mustakhbali wa baadaye.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akifunga hafla ya utiaji saini na kuridhia mkataba huo huku akitaja idadi ya nchi zilizotia saini mkataba huo.

(Sauti ya Ban).