Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Paris: Ban ki-moon ataka viongozi wasikilize sauti za vijana

Mkataba wa Paris: Ban ki-moon ataka viongozi wasikilize sauti za vijana

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Matiafa historia inaandikwa, viongozi wa nchi 171 za dunia wamekutana na wanatia saini mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi. Taarifa kamili na Amina Hassan

(TAARIFA YA AMINA)

Hivyo ndivyo mambo yalivyoanza katika uzinduzi wa kihistoria wa utiaji saini huo ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon baada ya kuwakaribisha viongozi na wawakilishi wa dunia katika hafla hii akamtambulisha na kumwachia jukwaa Gerturdue Clement, msichana wa miaka 16 kutoka Mwanza Tanzania akisema jamii ya kimataifa inapaswa kusikiliza sauti za vijana.

Gertrude akawahimiza viongozi kuchukua hatua leo, wala si kesho.

Kwa upande wake Bwana Ban amesema siku hii ni ya kihistoria katika jitihada za kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya vizazi vijavyo, wakati ambapo kila siku rekodi za uchafuzi wa hali ya hewa zinavunjwa.

Katibu Mkuu ameongeza kwamba ni lazima kusaidia nchi zinazoendelea kubadilisha chumi zao ili kuwa rafiki kwa mazingira akisema.

(Sauti ya Ban)

“ Tusisahau, hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi si mzigo, bali inaweza kuleta faidia nyingi. Inaweza kutusaidia kutokomeza umaskini, kuzalisha ajira, kutokomeza njaa, kuzuia mizozo na kuimarisha maisha ya wasichana na wanawake.”