Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka hatua zichukuliwe kukomesha ongezeko la kisukari duniani:

WHO yataka hatua zichukuliwe kukomesha ongezeko la kisukari duniani:

Idadi ya watu wanaoishi na kisukari imeongezeka takribani mara nne tangu mwaka 1980 na kufikia watu wazima milioni 422 wengi wao wanaishi katika nchi zinazoendelea..Amina Hassani na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

WHO inasema sababu kubwa ya ongezeko hili ni pamoja na uzito na unene wa kupindukia limetangaza leo shirika la adya duniani WHO katika kuelekea siku ya afya duniani ambayo huasdhimishwa kila mwaka April 7.

Kauli mbiu mwaka huu ni “shinda kisukari” na WHO imetoa wito kwa mataifa yote kuchukua hatua dhidi ya maradhi hayo. Katika ripoti yake ya kwanza kuhusu kisukari ambayo inainisha haja ya kuongeza juhudi za kuzuia na kutibu kisukari Etienne Krug, ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Magonjwa yasioambukizika, wa WHO anafafanua zaidi kuhusu ripoti hiyo.

(SAUTI YA DR ETIENNE)

"Ripoti hii inatoa wito wa kuchukua hatua. Ni wazi kwamba tunahitaji kusimamisha kasi ya ugonjwa huu, serikali zimetoa ahadi ya kusimamisha kasi hii, na kuhakikisha vifo vinavyozuilika kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanapunguzwa kwa asilimia 30 ifikapo mwaka 2030, na hii ni pamoja na kisukari."