Ban akaribisha matokeo mkutano wa nyukilia

2 Aprili 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha matokeo ya mkutano wa nyukilia wa  mwaka 2016 mjini Washington Marekani, akipongeza  tamko lililopitishwa na nchi shiriki pamoja na mpango mkakati katika kusaidia Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa ya msemaji wa ofisi yake, Ban amekaririwa akisema kuwa hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa mafanikio kupitia mchakato huo yatakuwa endelevu katika siku zijazo.

Ametaja maeneo ambayo yanahitaji kutiliwa mkazo ikiwamo uendelevu wa mahusiano ya ngazi ya juu ya kisiasa, kukuza mapendekezo ya uhusiano kati ya ugaidi wa kinyukilia na usalama wa mtandao na kwa jumuiya ya kimataifa, kuziba pengo kati ya kupokonywa silaha za nyukilia na kuzuia uenezwaji.

Jitihada za Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na changamoto ya kimataifa ya ugaidi wa nyukilia hutegemea nguzo mbili ambazo ni azimio la baraza la usalama namba 1540 (2004), nchi,viwanda na asasi za kiraia na wajibu wake katika mamlaka ili kuhakikisha nchi zote zinashughulikia changamoto hiyo na pili ni mkataba wa kimataifa kuhusu usimamamizi wa sheria ya ukandamizaji wa vitendo vya uagaidi wa kinyukilia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter