Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatathimini jukumu lake Ugiriki wakati muafaka wa Ugiriki na Uturuki waanza kutekelezwa:

UNHCR yatathimini jukumu lake Ugiriki wakati muafaka wa Ugiriki na Uturuki waanza kutekelezwa:

Mwishoni mwa wiki muafa kwa awali baina ya Uturuki na Muungano wa Ulaya wa kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaoingia Ugiriki na Ulaya umeanza kufanya kazi.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR tangu Jumamosi serikali ya Ugiriki imeanza kuharakisha uhamishaji hadi nchi kavu wa wakimbizi na wahamiaji wapatao 8000 waliowasili kisiwani kabla ya Machi 20.

Hatua hiyo ni kuwatenganisha na wale wanaowasili baada ya tarehje hiyo ambao watashughulikiwa kutokana na sera mpya ya kuwarejesha.

UNHCR inahofia kwamba muafaka huo wa EU na Uturuki unatekelezwa kabla ya mahitaji muhimu kuwa tayari nchini Ugiriki. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

“Kulingana na sera ya UNHCR ya kupinga kufungwa kwa wahamiaji, tumesitisha baadhi ya operesheni zetu katika vituo vya kufungia wakimbizi kwenye visiwa hivyo, vikiwemo kutoa usafiri hadi na  kutoka vituo hivyo. Hata hivyo tutabaki  kule ili kuendeleza shughuli za ulinzi na ufuatiliaji ili kujaribu kuhakikisha viwango vya haki za binadamu vinalindwa.”  

UNHCR imesema si sehemu ya muafaka huo na haitahusika na kuwarejesha wakimbizi na wahamiaji na vituo wanakowekwa.