Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW60 yajadili umuhimu wa maji

CSW60 yajadili umuhimu wa maji

Leo ikiwa ni siku ya maji duniani mjadala kuhusu umuhimu wa maji na huduma za kujisafi umegubika katika mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW60 .

Katika moja ya mikutano ya ndani uliojadili kwa kina kuhusu upatikanaji wa maji na huduma za kujisafi ambayo ni lengo namba sita la maendeleo SDGS, Emem Okon mwasisi wa shirika la maendeleo ya rasilimali za wanawake nchini Nigeria liitwalo Kebetkache na ambalo limejikita katika bonde la mto Niger, ameuambia mkutano huu.

( SAUTI)

‘‘Ikiwa ni matokeo ya shughuli za viwanda, mashirika ya kimataifa yamechangia pakubwa katika kuharibu upatikanaji wa maji hasa kwa wanawake. Sio tu kuathiri wanawake kukosa maji bali pia ustawi wao kwani katika bonde la mto Niger kazi ya msingi ya wanawake hususani vijijini, ni uvuvi na kilimo.’’

Wanaharakati mbalimbali kuhusu haki ya maji kutoka sehemu mbalimbali duniani wamezungumzia umuhimu wa huduma hiyo ambapo wamesema ni mtambuka katika maendeleo endelevu.