Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nitahakikisha wasichana Tanzania wanafikiwa na elimu nilioipata: Mshiriki CSW60

Nitahakikisha wasichana Tanzania wanafikiwa na elimu nilioipata: Mshiriki CSW60

Miongoni mwa wasichana wanaohudhuria mijadala ya mkutano wa sitini wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW60 unaoendelea jijini New York ni Caroline Philemon kutoka Tanzania anayewakilisha taasisi ya kimataifa ya  kanisa katoliki Grail.

Caroline ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari mtakatifu Teresia wa Avila ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa atakaporejea nyumbani atahakikisha uzoefu na kile alichojifunza kinawafikia wasichana wenzake.

(SAUTI CAROLINE)

Caroline anataja kile kinachosukuma kufanya uwakili kwa wanawake na wasichana.

(SAUTI CAROLINE)