Skip to main content

Kuwezesha wanawake kifedha kutachangia maendeleo kwa ujumla- Josee Ntabahungu

Kuwezesha wanawake kifedha kutachangia maendeleo kwa ujumla- Josee Ntabahungu

Kikao cha 60 cha Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake (CSW60) kikiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, serikali na sekta binafsi zimeshauriwa ziwasaidie wanawake kwa kuwawezesha kifedha.

Josee Ntabahungu, Meneja wa Programu ya Kuendeleza Wanawake katika Shirika la Care International, nchini Burundi amekiambia kikao cha jopo la ngazi ya juu kwamba kuna haja ya ushirikiano katika uratibu na uwekezaji katika miradi ya wanawake ili kuwawezesha wanawake kifedha.

Amesema kufanya hivyo kutachangia maendeleo siyo tu katika maisha ya wanawake hao binafsi, lakini pia katika jamii na nchi  kwa ujumla.

Sauti ya Josee Ntabahungu