Vifo vitokanavyo na homa ya Lassa nchini Benin vyaongezeka
Idadi ya vifo vya wagonjwa watokanao na homa ya Lassa nchini Benin imeongezeka na kufikia 17 huku visa 52 vikishukiwa , hii ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF ambayo yanasaidia kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Assumpta Massoi na taarifa kamili
(TAARIFA YA ASSUMPTA)
Hili ni ongezeko la vifo vya watu watano ikilinganishwa na taarifa ya awali ya WHO na UNICEF iliyokariri vifo 12 huku pia ongezeko mara mbili likiwa katika ambapo awali taarifa zilidai kuwa hilo lilidai kuwa watu 25 wanashukiwa kukumbwa na virusi vya homa ya Lassa ambavyo husambazwa kwa binadmu kwa njia kadhaa ikiwamo kupitia damu na mkojo.
Katika taarifa ya pamoja mashirika hayo yameelezea kuwa miongoni mwa visa vilivyothibitishwa ni mtoto mwenye umri wa miaka minne anayetibiwa hivi sasa kaskazini mashariki mwa taifa hilo .
Kwa kushirikiana na wadau wa afya na misaada ya kibinadamu , na serikali ya Benin, hatua za dharura zinaendelea kuchukuliwa kuzuia kuenea kwa virusi vya homa ya Lassa ambavyo viligundulika mezi Januari baada ya mwanamke mjamzito aliyekuwa na dalili za homa hiyo lufariki na kufuatiwa na kisha wahumdumu wengine wa afya sita kufariki katika hospitali moja katikatia mwa Benin