Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matukio yoyote ya ghasia na uchochezi CAR wakati wa uchaguzi yataorodheshwa: Bensouda

Matukio yoyote ya ghasia na uchochezi CAR wakati wa uchaguzi yataorodheshwa: Bensouda

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Bi Fatou Bensouda ameionya Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambayo itapiga kura siku ya Jumapili tarehe 27 Desemba kuwa matukio yoyote ya ochochezi na ghasi wakati wa uchaguzi yataorodheshwa.Flora Nducha na taarifa kamili.

(Taarifa ya Flora)

Wananchi wa CAR Jumapili watapiga kura kuchagua Rais na wabunge. Bi Bensouda amesema kwa mamlaka aliyonayo na kuzingatia mkataba wa Roma anafuatilia kwa karibu hali nchini CAR,na kusema ingawa kura ya maoni ya karibuni ilivutia wapiga kura wengi licha ya machafuko yanayoendelea , anatiwa hofu na taarifa za matukio ya ghasia na vitisho katika juhudi za kuwavuruga wapiga kura wasijitiokeze.

Amesema ghasia kama hizo zinaweza kuwa ni uhalifu kwa mujibu wa vipengee vya mahakama ya ICC na hivyo ni lazima zikome mara moja na kuongeza kuwa mchakato wa kukusanya ushahidi dhidi ya watu wanaochochea au kujihusisha na ghasia kabla, wakati na baada ya uchaguzi unaendelea, huo ni uhalifu na mahakama ya ICC itaushughulikia.