Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa maazimio ni siri ya kutokomeza Polio Tanzania: Dk Mbando

Utekelezaji wa maazimio ni siri ya kutokomeza Polio Tanzania: Dk Mbando

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la afya ulimwenguni WHO, pamoja na la kuhudumia watoto UNICEF hivi karibuni yametangaza kuwa Tanzania imefanikiwa kutokomeza ugonjwa Polio unaosababisha kupooza kwa viungo vya mwili.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, mafanikio hayo yanatokana na utashi na uongozi thabiti wa taifa hilo pamoja na ushirikiano kati yake na wadau wa afya ikiwamo ubia wa chanjo duniani GAVI.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Katibu Mkuu wa wizara ya afya Tanzania Dk Donan Mbando anaeleza kile ambacho kimefanywa ili kufikia hatua hiyo.

(SAUTI DK MBANDO)

Kadhalika akashauri nchi nyingine zifanye nini kufikia mafanikio hayo..

(SAUTI MBANDO)