Skip to main content

Muafaka Cop21 ni muhimu saana katika kuokoa maisha:Schwarzenegger

Muafaka Cop21 ni muhimu saana katika kuokoa maisha:Schwarzenegger

Katika wiki ya pili ya mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya ataibia nchi Cop21 mjini Paris Ufaransa , watu mbalimbali mashuhuri na wanaharakati wamekuwa wakipaza sauti zao kuchagiza muafaka wa kukabiliana na mabadiliko ya taibia nchi.

Miongoni mwao ni Arnold Schwarznegger ambaye pia ni mcheza filamu maarufu. Ametoa wito kwa Cop21 kuafikiana na kukomesha vifo milioni 7 vinavyohusiana na uchafuzi wa hali ya hewa kila mwaka.

(SAUTI YA ARNOlD SCHWARZENEGGER)

“Nafikiri ni muhimu kufikia makubaliano kwa sababu ni haki ya dunia! Na hii ni lazima ikome, kuwa na watu Milioni Saba wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na uchafuzi.”