Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea COP21 FAO yatoa tahadhari kwa hatua kwa sekta ya kilimo

Kuelekea COP21 FAO yatoa tahadhari kwa hatua kwa sekta ya kilimo

Ukame, mafuriko, vimbunga na majanga mengine yaliyochochewa na mabadiliko ya tabianchi yameongezeka kwa kasi kubwa miongo mitatu iliyopita na hivyo kutishia uhakika wa chakula katika nchi zinazoendelea kwa kuwa majanga hayo yalizidi kuathiri sekta ya kilimo. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO iliyotolewa leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 huko Paris, Ufaransa wiki ijayo.

Ikijikita zaidi kwenye athari za mabadiliko ya tabianchi yatokanayo na majanga asili kwenye nchi zinazoendelea, ripoti inasema asilimia 25 ya madhara hayo ilikuwa kwenye mazao, mifugo, uvuvi na misitu pekee na kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo hakuna hatua zinachukuliwa.

Dominique Burgeon ni Mkurugenzi wa FAO kitengo cha masuala ya dharura.

(Sauti ya Dominique)

“Kwa ujumla sekta ya kilimo haizingatiwi vya kutosha iwe suala la usaidizi wa kibinadamu au kupunguza athari za majanga. Tunafahamu vyema kuwa pesa inayowekezwa kwenye kupunguza athari za majanga, inawezesha kupunguza kwa kiasi kubwa gharama pindi janga linapotokea.”