Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajasiriamali wanawake waangaziwa

Wajasiriamali wanawake waangaziwa

Katika kuadhimisha siku ya wajasiriamali wanawake hii leo, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mjadala ukiangazia masuala nyeti yanayoathiri kundi hilo hususan nafasi ya serikali kuchagiza sekta hiyo.

Katika mjadala huo washiriki wamesema wajasiriamali wanawake wanakumbwa na vikwazo katika kupata mitaji na masoko ya bidhaa zao licha ya kwamba takwimu zinaonyesha kuwa biashara zinazoongozwa na wanawake zitakua kwa asilimia 90 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Miongoni mwa walioshiriki kwenye jopo la mjadala huo ni mwakilishi wa kudumu wa Panama kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi   Laura Flores ambaye amesema serikali zina dhima muhimu kwani zinatunga sera.

(Sauti ya Balozi Laura)

“Katika uhalisia huu hatuwezi kuacha nyuma asilimia 50 ya idadi yote ya watu, ni muhimu kusonga mbele kwa ajili ya maendeleo. Kwa hiyo ni jambo tunalolitazama kwa kina hapa Umoja wa Mataifa na kuweka mwongozo na ni matumaini yetu kuwa serikali zitazingatia na kutekeleza ajenda hii katika ngazi ya kitaifa na nyinginezo.”