#WRC15 yaendelea Geneva, nchi za Afrika ziko makini:

6 Novemba 2015

Mkutano mkuu wa dunia kuhusu masafa ya mawasiliano ya radio umeingia siku ya Tano huko Geneva, Uswisi ukiwa na lengo la kuangalia upya sera kuhusu mgao na matumizi ya masafa. Masafa hurahisisha mawasiliano mbali mbali ikiwemo yale ya simu ziwe za mkononi au mezani, safari za anga, matangazo ya radio, televisheni na hata mitandao ya intaneti.Mkutano huo umeandaliwa na shirika la mawasiliano duniani, ITU ambalo Tanzania ni moja ya nchi wanachama. Ili kufahamu lengo hasa la mkutano huo, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na mjumbe kutoka Tanzania, Innocent Mungy ambaye pia ni Meneja mawasiliano kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA na anaanza kwa kuelezea ajenda kuu sanjari na masuala yanayozua mjadala mkubwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter