Kutoka Daadab, marejeo ni Somalia baada ya amani kuanza kurejea

Kutoka Daadab, marejeo ni Somalia baada ya amani kuanza kurejea

Daadab, kambi ya wakimbizi iliyoko kwenye kaunti ya Garissa nchini Kenya, inahifadhi wakimbizi wengi wao kutoka Somalia. Machafuko nchini humo yaliyofuatia kupinduliwa kwa serikali ya Said Barre mwaka 1991 yalisababisha raia wengi kukimbia makwao. Hata hivyo hivi sasa harakati za kurejesha amani zinazochagizwa na pande mbali mbali ikiwemo Umoja wa Mataifa zimeanza kuzaa matunda na wananchi wanaanza kurejea nyumbani kwa hiari.

Je hali inakuwaje? Tunaanzia kambini Daadab, na anayetupeleka ni Grace Kaneiya kupitia makala hii.