Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

NEPAD ni fursa ya kufanikisha SDGs na ajenda 2063 ya Afrika: Abdelaziz

NEPAD ni fursa ya kufanikisha SDGs na ajenda 2063 ya Afrika: Abdelaziz

Maadhimisho ya wiki ya Afrika ndani ya Umoja wa Mataifa yanaendelea leo jijiini New York, Marekani kwa shughuli mbali mbali ikiwemo utoaji wa taarifa kuhusu mpango wa Afrika kujitathmini  yenyewe, APRM na ule wa ubia wa maendeleo, NEPAD.

Wakati hayo yakiendelea, Msaidizi wa Katibu Mkuu na mshauri wake kuhusu Afrika Maged Abdelaziz amesisitiza kuwa NEPAD ni mojawapo ya fursa za kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu, SDG na ile ya maendeleo Afrika 2063.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa..

(SAUTI)

'Kukuza maelewano, mshikamano katika utekelezaji wa mipango miwili hiyo na kuhakikisha kwamba mikakati miwili inasaidiana . Ndiyo maana tumekuwa na mikutano mikuu kadhaa ikiwamo wa biashara huria, na ule wa kukomesha mitutu ya bunduki''.