Skip to main content

Uchaguzi wa wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama ni leo

Uchaguzi wa wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama ni leo

Uchaguzi wa wanachama watano wasio wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unafanyika leo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Nafasi za wawakilishi hao watano zitagawanywa kikanda, mbili zikendea bara Afrika, ambalo sasa linawakilishwa na Chad na Nigeria, moja kwa Asia na nchi ndogo zinazoendelea za visiwa vya Pasifiki, ambayo sasa inashikiliwa na Jordan, kiti kimoja kwa nchi za Amerika ya Kusini na Karibi, kikishikiliwa sasa na Chile, na hatimaye, nafasi moja kwa nchi za Mashariki mwa Ulaya, ambayo sasa inashikiliwa na Lithuania.

Nchi zinazowania nafasi hizo ni Japan kwa Asia, Misri na Senegal kwa kanda ya Afrika, Ukraine kwa kanda ya Wilaya Mashariki, na Uruguay kwa kanda ya Amerika Kusini na Karibi.

Wagombea katika uchaguzi wa leo wanatarajiwa kuchaguliwa bila kupingwa, kwani hawana washindani kutoka kanda zao. Wanachama wasio wa kudumu hushiriki kupiga kura, inagawa hawana kura ya turufu.