Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii Nane zawa mabingwa wa kukabili majanga

Jamii Nane zawa mabingwa wa kukabili majanga

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa majanga, UNISDR imetangaza jamii nane kuwa mabingwa wa kukabiliana majanga.

Jamii hizo zinazoishi kwenye maeneo hatari ya kukumbwa na mafuriko, vimbunga, matetemeko ya ardhi na milipuko ya volcano zinatoka Bangladesh, Cameroon, Colombia, Italia, Uingereza, Ufilipino, Sudan na Vanuatu.

Mkuu wa UNISDR Margareta Wahlström amesema wametambua jamii hizo kutokana na uwezo wao wa kutumia mbinu za kijadi na kiasili kukabiliana na majanga, wakati huu ambapo leo ni siku ya kukabiliana na majanga duniani.

Amesema siri kuu ya jamii hizo ni utangamano wa kijamii ambao unaziunganisha na kuweza kupunguza madhara yatokanayo na majanga.

Bi. Wahlström amesema maendeleo endelevu na utokomezaji wa umaskini haviwekezani bila jitihada za kudhibiti majanga.