Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuweke ajenda ya haki ya wanawake kuongoza iwe juu: Ban

Tuweke ajenda ya haki ya wanawake kuongoza iwe juu: Ban

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala kuhusu nafasi ya wanawake katika amani na usalama duniani likijikita zaidi katika azimio namba 1325 la baraza hilo lililopitishwa miaka 15 iliyopita. Assumpta Massoi amefuatilia mjadala huo.

(Taarifa ya Assumpta)

Mjadala uliongozwa na Waziri Mkuu wa Hispania Mariano Rajoy ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema miaka 15 baada ya kupitishwa kwa azimio hilo linalosisitiza uhusiano thabiti kati ya usawa wa kijinsia na amani na usalama duniani, kuna mafanikio ikiwemo ushiriki wa wanawake kuongoza harakati za kuondokana na ukatili wa kingono, lakini bado vikwazo vinazidi kuzuia kuchanua kwa wanawake kutekeleza wajibu wao kwenye suala hilo.

(Sauti ya Ban)

“Wakati vikundi vyenye misimamo mikali vikiweka ukandamizaji wanawake kuwa ajenda yao ya juu, ni lazima tuweke haki ya uongozi na ulinzi wa wanawake kuwa ajenda yetu kuu.”

Phumzile Mlambo-Ngucka, Mkuu wa UN-Women amesema misimamo mikali ni changamoto mpya kwa haki za wanawake hivyo..

(Sauti ya Phumzile)

“Kuongeza kwa asilimia 15 lengo la uchangiaji wa fedha za  ujenzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya miradi ya kushughulikia ghasia zinazotokana na misimamo mikali.”