Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana changamkieni ubaharia #CareerAtsea: IMO

Vijana changamkieni ubaharia #CareerAtsea: IMO

Ubaharia, taaluma ambayo kwa sasa inaonekana kuyoyoma na vijana wengi kuikwepa licha ya kuchangia kwa kiasi kikubwa katika biashara duniani. Takwimu za kiuchumi kutoka shirika la kimataifa la masula ya bahari, IMO zinasema kuwa asiilmia 90 ya biashara hiyo inatokana na bidhaa zinazosafirishwa kwa meli. Licha ya umuhimu huo, bado wafanyakazi wanaoshinda kutwa kucha kwenye meli hizo wakipitia safari za majini za muda mrefu bado ushujaa wao hautambuliki na idadi yao inapungua. Ni kutokana na hali hiyo, IMO imeamua kutumia siku ya kimataifa ya baharia tarehe 25 mwezi Juni mwaka huu kushawishi vijana kujiunga na taaluma hiyo ambayo IMO inasema ni zaidi ya ajira. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi amezungumza kwa njia ya simu na Msimamizi wa kitengo cha Kiingereza cha idara ya mikutano ya IMO Irene Waite kutoka London, Uingereza ambapo anaanza kwa kuelezea lengo la kampeni hii.