Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati ni huu wa kubadili fikra; wanawake wanaweza: Bi. Nducha

Wakati ni huu wa kubadili fikra; wanawake wanaweza: Bi. Nducha

Siku ya Radio duniani imeadhimishwa tarehe 13 Februari ambapo Kaimu Mkuu wa Radio ya Umoja wa Mataifa Bi. Flora Nducha amesema wakati umefika kwa wasikilizaji kutambua kuwa wanawake wanaweza na kwamba radio ikitumika vyema inaweza kuleta mabadiliko ya kifikra ambayo yamekuwa yakikwamisha ari ya wanawake na hata wanaume kupatia kipaumbele kundi hilo. Katika mahojiano nami  Joseph Msami kuhusu siku hiyo adhimu amesema Radio ya Umoja wa Mataifa kupitia idhaa zake zote Nane zinazotangaza kila siku na nyingine Tatu zinazotangaza kwa wiki, imetumia siku ya Radio kueneza ujumbe huo na hapa anaanza kwa kutoa wito kwa wasikilizaji.