Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia sakata la Al Bashir na ICC

Ban azungumzia sakata la Al Bashir na ICC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa huko Geneva, Uswisi kwa ajili ya mashauriano kuhusu Yemen amezungumzia sakata la kutakiwa kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar Al Bashir ambaye wiki hii alikuwepo huko Afrika Kusini kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Muungano wa Afrika. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC ilitoa hati za kukamatwa kwa Al Bashir lakini hadi sasa hajakatwa na hata akiwa mkutano huko Afrika Kusini hakukamatwa licha ya mahakama hiyo kutaka akamatwe. Katika mkutano na waandishi wa habari huko Geneva, kando vya vikao kuhusu Yemen Ban akaulizwa kuhusu kutokamatwa kwa Al Bashir.

(Sauti ya Ban)

“Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, imetoa amri ya kukamatwa kwa rais Al bashir kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na wa kivita, na ni jambo ambalo nalipa kipaumbele sana, Mamlaka ya ICC ni lazima iheshimiwe, na ni uamuzi wake utekelezwe.”