Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya Sudan Kusini yamininisha wakimbizi zaidi nchi jirani

Mapigano mapya Sudan Kusini yamininisha wakimbizi zaidi nchi jirani

Mapigano makali kwenye majimbo ya Unity na Upper Nile nchini Sudan Kusini katika kipindi cha miezi miwili iliyopita yamesababisha zaidi ya watu Laki Moja kupoteza makazi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR likisema kama hiyo haitoshi misaada ya kibinadamu kwa watu Laki Sita na Nusu haiwezi kuwafikia kwa kuwa mashirika ya misaada yamelazimika kujiondoa.

Kwa mantiki hiyo wakimbizi wamemimnika nchi jirani ikiwem 30,000 Sudan, 15,000 Ethiopia na hivyo kufanya idadi ya wananchi waliokimbilia nje ya nchi yao tangu mzozo kuzuka Disemba 2013 kufikia 550,000 huku Milioni Moja na Nusu wakisalia wakimbizi wa ndani.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR Geneva  anasema wajiandaa kwa hali mbaya zaidi kwa kuwa..

 (Sauti ya Adrian).

“Wakimbizi wanataja ongezeko la mapigano na  ukosefu wa uhakika wa chakula kuwa sababu za kukimbia makazi yao. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu Milioni Tatu nukta Nane ambao ni Theluthi moja ya wananchi wote Milioni Kumi na Moja wa Sudan Kusini hawana chakula cha kutosha.”

UNHCR inasema pamoja na idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini kuongezeka, ina hofu pia na mchango wa ombi maalum la usaidizi wan chi hiyo kwa mwaka 2015 ambalo hadi sasa limechangiwa kwa asilimia 10 tu.