Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi: Maabara Maweni yaimarishwa kudhibiti Kipindupindu

Wakimbizi wa Burundi: Maabara Maweni yaimarishwa kudhibiti Kipindupindu

Shirika la afya duniani, WHO limeongeza uwezo wa vifaa na watendaji kwenye hospitali ya mkoa wa Kigoma, Maweni nchini Tanzania ili kuimarisha uwezo wake wa kuchunguza mlipuko wa kipindupindu.

Mlipuko huo wa mwezi uliopita ulitokana na mminiko mkubwa wa wakimbizi wa Burundi uliosababishwa na ukosefu wa maji na mazingira safi.

Miongoni mwa watendaji waliopelekwa ni mtaalamu wa maabara Jacob Lusekelo ambaye anaelezea wanachofanya kubaini kwa ufasaha bakteria wanaosababisha kipindupindu.

(Sauti ya Jacob)

“Ilikupata matokeo ya kweli tunachukua samuli ya choo cha mgonjwa kuchunguza bakteria na kuona ni dawa gani inafaa kutibu na matokeo hubainika ndani ya saa 48. Kuna awamu tatu: Kuandaa vitendanishi,kutenga na kutambua vimelea, na mwisho matokeo kutolewa na kutupa kinyesi. Kisa cha kipindupindu kinathibitishwa wakati bakteria wa Kipindipundu anapobainika kwenye choo cha mgonjwa anayehara.”

.”