Skip to main content

Waasi 442 wa FRPI huko Ituri DRC waamua kujisalimisha

Waasi 442 wa FRPI huko Ituri DRC waamua kujisalimisha

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa  nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC umekaribisha tangazo la waasi wa kikundi cha Ituri Resistance Patrioti Front, FRPI la kujisalimisha kwa amani.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema tayari hapo jana waasi 442 wa kikundi hicho walisema wako tayari kujisalimisha ambapo kundi la wanaume wenye silaha wakiwa na wanawake na watoto walijikusanya kwenye mji wa Ituri ulioko Mashariki mwa nchi hiyo.

Hivi sasa MONUSCO inahakikisha ulinzi na usaidizi wa kiufundi kwa serikali ya DRC ili kufanikisha zoezi hilo.