Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu chathibitishwa miongoni mwa wakimbizi wa Burundi Nyarugusu:UNHCR

Kipindupindu chathibitishwa miongoni mwa wakimbizi wa Burundi Nyarugusu:UNHCR

Wakati raia wa Burundi wakiripotiwa kuzidi kumiminika nchi jirani kusaka hifadhi kutokana na sintofahamu nchini mwao, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Tanzania limethibitisha visa 13 vya ugonjwa wa kipindupindu kwenye kambi ya Nyarugusu inayohifadhi wakimbizi hao. Thibitisho hilo linakuja siku moja tu baada ya shirika hilo kutangaza vifo vya wakimbizi Saba kutokana na ugonjwa wa kuhara.Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats..

Ni mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania Joyce Mends-Cole akizungumzia taarifa hizo ambapo amesema wagonjwa 13 wamethibitika kati ya sampuli za wagonjwa 77 zilizowasilishwa maabara kwa uchunguzi. Ametaja hatua wanazochukua kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo unaoambukiza haraka.

(Sauti ya Joyce)

“Tunahakikisha tuna dawa za kutosha. Tumeomba serikali ifungue bohari yake tupate dawa na malori yetu yanaondoke Dar es salaam yakiwa na dawa.Najua WHO imesema italeta dawa kutoka nje ya Tanzania na UNHRC imeomba msaada kutoka MSF Ubelgiji najua watafika punde kutusaidia kinga na tiba. Na pia tunaweka dawa za kutakasa kwenye boti zinazosafirisha wakimbizi.”

Miongoni mwa wakimbizi ni mwanamke aliyejifungua kwa upasuaji nchini Burundi lakini alikimbia kwa hofu ya machafuko na sasa UNHCR..

(Sauti ya Joyce)

“Alikuja na mshono hivyo tuliweza kumhamishia hospitali kutoka Kagunga. Hivyo naamini hapa tunajitahidi kushughulikia ujauzito na kujifungua.”

Kutoka kambini Nyarugusu mume wa mwanamke mmoja aliyejifungua kwenye boti anasimulia kilichowakumba.

(Sauti ya Mume)

UNHCR inatoa wito kwa usaidizi zaidi wa kifedha ili kufanikisha usafirishaji wa wakimbizi hao kutoka Kagunga kwenda kambi ya Nyarugusu ikisema gharama ya msafara mmoja wa boti ni dola 10,500 za kimarekani na kwa siku boti moja inafanya safari mbili tu.