Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia yaongoza kwa uwekezaji: UNCTAD

Asia yaongoza kwa uwekezaji: UNCTAD

Nchi zinazoendelea zilizoko katika ukanda wa Asia zimemewekeza fedha nyingi nje ikilinganishwa na zile za Amerika ya Kaskazini na Ulaya imesema kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Taarifa ya UNCTAD kwa vyombo vya habari inasema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa kufikiwa kwa rikodi hiyo ikisema kuwa awali mji wa Hong Kong na China ilikuwa nchi ya pili na ya tatu kwa uwekezaji baada ya Marekani ambayo inasalia kuwa chanzo kimoja cha uwekezaji wa nje moja kwa moja (FDI).

Katika nchi kuu 20 kwa uwekezaji duniani, tisa zilikuwa ama kutoka mataifa yanayoendelea au zenye uchumi wa mpito imesema ripoti hiyo.

UNCTAD imesema kuwa mwaka 2014 mashirika ya kimataifa kutoka katika mataifa yanayoendelea pekee yaliwekeza dola nusu trillioni nje ikiwa ni nyongeza ya asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka jana.