Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea juma la chanjo duniani, watoto milioni 1.5 waweza kuokolewa: WHO

Kuelekea juma la chanjo duniani, watoto milioni 1.5 waweza kuokolewa: WHO

Kuelekea juma la chanjo duniani shirika la afya ulimwenguni WHO linasema misha ya watoto milioni moja na nusu yangeweza kuokolewa ikiwa wangepatiwa  chanjo mujarabu. Tarifa ya Grace  Kaneiya inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa mujibu wa WHO chanjo ambayo ingeweza kuokoa maisha ya watoto hao ni dhidi ya magonjwa ambayo huwashambulia mara kwa mara ikiwamo dondakoo na pepounda

Dk Jean-Marie Okwo-Bele, ni mkuu wa kitengo cha chanjo WHO anaeleza kwanini idadi kubwa ya watoto hawapati chanjo

(SAUTI DK BELE)

Hawapati chanjo hizi kwasababu ama hawafikiwi na  mifumo ya afya au wakati wanakwenda katika vituo vya afya hakuna huduma hizi. Wengine huishi katika maeneo yenye machafuko kwahiyo wahudumu wa afya  na huduma hazipatikani mara kwa mara.

Chanjo inafahamika kama njia bora ya tiba na rahisi inayozuia vifo takribani milioni tatu kila mwaka.