Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

PAM yasambaratisha zaidi ya asilimia 80 ya shule huko Vanuatu

PAM yasambaratisha zaidi ya asilimia 80 ya shule huko Vanuatu

Kimbunga PAM kilichopiga hivi karibuni nchi ya Vanuatu kimeripotiwa kuathiri takribani watu 166,000 kwenye visiwa 22 vilivyopo nchini humo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema idadi hiyo ya waathiriak ni pamoja na watoto 82,000 ambao sasa hawawezi kwenda shule kutokana na shule zao kusambaratishwa au kugeuzwa makazi ya kimbilio kwa waathirika wa kimbunnga hicho.

Kwa mantiki hiyo imeanzisha vituo vya muda vya mafunzo na kupeleka vifaa vya shule.

Wakati takribani watu 4,000 bado wamesalia kwenye vituo vya dharura kwenye mji mkuu Port Villa wakihitaji vyakula, malazi na maji safi na salama, UNICEF imesema inapeleka pia misaada kukidhi mahitaji hayo wakati huu ambapo makinga maji ya mvua yameharibiwa.

Hata hivyo UNICEF imesema imenaza kutoa misaada lakUNICEF inaonya uwezekanao wa mlipuko wa magonjwa kutokana na mafuriko, mazingira duni ya kiafya na mkwamo kwenye huduma za afya.