Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misemo ya wahenga yadhihirika kambini Kyangwali nchini Uganda

Misemo ya wahenga yadhihirika kambini Kyangwali nchini Uganda

Wahenga walisema penye nia pana njia na kama haitoshi haba na haba hujaza kibaba! Misemo hiyo imedhihirika huko kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda ambako mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Sudan Kusini licha ya kuishi mazingira magumu, ametumia fursa zilizokuwa zinamzingira kubadili siyo tu maisha yake bali na ya jamii inayomzunguka.

Je amefanya nini? Ungana na John Kibego kutoka nchini Uganda.